Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema mwaka wa 2019 ni mwaka sahihi kwa upimaji wa Tezi Dume ambapo hadi uchaguzi wa Serikali wa Mitaa na Uchaguzi mkuu unapofika 2020 kusiwe na ugonjwa huo.
RC Makonda ameyasema hayo wakati akizinduzi kampeni maalum kuhusu afya ya uzazi ambapo amesema mchakato huo utawahusisha wanawake kwa wanaume, ikiwezekana kuwafata watu majumbani mwao kama hawataki kufika vituo vya afya kupimwa.
“Mchakato huu niliusema kipindi kile watu wakafurahi kwa sababu wanahamishiwa Dodoma kama ni mwananchi wa Dar es Salaam tutakufata hata Dodoma upimwe, tusingependa uende mkoa mwingine ukiwa unaumwa, ugonjwa huu ni hatari na unamaliza watu wengi sana,“amesema.