Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli leo October 19 2018 alikutana na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais amekutana nao na kula nao chakula cha mchana sambamba na kuwachangia pesa.
Kabla ya kula nao chakula cha mchana Rais Magufuli aliongea na wachezaji hao na kuwahasa mambo muhimu yatakayowasaidia katika maisha yao ya soka, sambamba na kuchangia Tsh Milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Taifa Stars.
“Nilikuwa naambiwa mnajiandaa kwenda Lesotho si ndio mimi nitachangia Tsh Milioni 50 ambazo nataka ziende zikatumike kwa Watu wanaostahili”- Rais Magufuli
Rais JPM alivyowaita Taifa Stars Ikulu “Tukishindwa mtazitapika”
Samatta alivyofutwa miguu baada ya game