Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kinatarajia kufanya uchaguzi kumchagua Rais mpya wa chama hicho pamoja na Makamu Rais katika uchaguzi utakaofanyika April 14, 2018 ambapo kwa sasa Rais wao ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu ambae yupo katika matibabu Ubelgiji.
Walioteuliwa kuwania nafasi hiyo na Kamati ya uchaguzi ya TLS ni Fatma Karume, Makamu wa Rais wa sasa, Godwin Ngwilimi, Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga.
Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi Dr. Kibuta Ongwamuhama imempitishwa Rugemeleza Nshalla kugombea nafasi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa EAC Kenya ameeleza jinsi Tafiti zinavyoibiwa