Kiungo wa zamani wa Man City Yaya Toure ameamua kufunguka na kuzungumzia uwezo wa kiungo wa Man United Paul Pogba, ambaye hivi karibuni amekuwa gumzo kubwa kutokana na kuonesha uwezo mkubwa zaidi baada ya kuondoka kwa kocha Jose Mourinho katika club ya Man United.
Pogba amekuwa na wakati mzuri kwa sasa chini ya kocha mpya wa mpito Ole Gunnar, kwani katika game sita alizocheza chini ya Kocha huyo amefunga magoli 4, mengi zaidi ya alivyokuwa chini ya kocha Jose Mourinho ambapo ilidaiwa kuwa wawili hao hawakuwa katika wakati mzuri.
“Nafikiri Paul kwa sasa anaaminiwa sana na kocha wake ana uwezo wa kufanya anachokifanya nafikiri kama ulimuangaliwa wakati wa Kombe la Dunia Urusi utanielewa maana ule ulikuwa ni mfano mzuri, tulikuwa tunaona baadhi ya clip video zikimuonesha anavyoongea na wachezaji wenzake katika vyumba vya kubadilishia nguo”>>>Yaya Toure
Hata hivyo Toure aliongeza kwa kutoa onyo kwamchezaji huyo kuhusiana na baadhi ya watu kumkosoa na kusema kuwa masuala hayo hayakwepeki tu “Kuhusu kukosolewa kwake hiyo ipo tu siku zote lakini ni mchezaji professional lakini unatakiwa uikubali na kufanya kazi kwa bidii ndicho anachokifanya Pogba sasa” >>> Yaya Toure
Mpenja kata ngaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake