Usiku wa May 13 2018 katika mji wa Valencia nchini Hispania club ya Levante FC licha ya kuipokea FC Barcelona kwa heshima ambao ndio Mabingwa wa LaLiga msimu huu 2017/2018 pamoja na kuwawekea guard of honour lakini haikuwaacha waondoke salama katika mji wa Valencia.
Levante wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuhakisha wanavunja rekodi ya FC Barcelona msimu wa 2017/2018 ambapo club hiyo ilikuwa inadhamiria kumaliza Ligi pasipo kupoteza mchezo wowote, Levante wakiwa nyumbani leo wamefanikiwa kuiadhibu FC Barcelona kwa magoli 5-4, hivyo na kuifanya club yao ndio kuwa timu ya kwanza kuchukua point tatu LaLiga dhidi ya Mabingwa wa Ligi hiyo FC Barcelona.
Magoli ya Levante yalifungwa na Boateng dakika ya 9, 31 na 49, Bardhi dakika ya 46 na 56 wakati magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Philippe Coutinho aliyefunga hat-trick dakika ya 39, 59 na 64 huku goli la nne likifungwa na Luis Suarez kwa penati dakika ya 71, Barcelona ni miongoni mwa vilabu vichache duniani ambavyo vimetangazwa Mabingwa bila kufungwa lakini wameshindwa kulinda rekodi ya kumaliza msimu pasipo kupoteza mchezo.
Vilabu karibia vyote Ulaya na duniani kwa ujumla vimechukua Ubingwa wa Ligi zao lakini vimepoteza mchezo msimu huu, hivyo sasa kwa Tanzania kazi inabaki kwa Simba SC ambao ndio Mabingwa wa Tanzania bara kama wataweza kumaliza msimu bila kupoteza mchezo kwani nao wamesalia na game mbili dhidi ya Kagera Sugar na game dhidi ya Majimaji FC wataweza kujilinda wasipoteza?
Simba kama Man City tu wametwaa Ubingwa wa Ligi nje ya uwanja leo