Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines Jumatano ya Septemba 14 ni kuhusiana na kocha wa Man United Jose Mourinho kuamua kumuacha nahodha wa Man United Wayne Rooney katika safari ya kwenda Uholanzi kucheza na Feyenoord katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi A hatua ya Makundi ya Europa League.
Jose Mourinho akiwa katika mkutano na waandishi wa habari Uholanzi kuelekea mchezo huo utakaochezwa usiku wa leo Septemba 15 ameweka wazi sababu za kwa nini kamuacha Wayne Rooney katika kikosi cha wachezaji wa Man United waliosafiri kwenda Uholanzi akiwa sio majeruhi na alifanya mazoezi ya mwisho pamoja na timu.
“Rooney nimemuacha kwa sababu amecheza dakika 90 za kila mchezo toka umeanza msimu akiwa United na England lakini amecheza dakika 90 mechi iliyopita hivyo nimetaka apumzike arefresh kwa ajili ya mechi ijayo, ndio maana hata Valencia na Shaw hajasafiri na timu nataka niwe na kikosi imara leo na katika mchezo wa weekend”
https://youtu.be/Vq2EBuSIAaQ
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0