Ikiwa ni Februari 28, 2019 tunayo story ya kusikitisha kuhusu kuteketea kwa moto katika ghala la kuhifadhia vifaa vya Ujenzi katika kiwanda cha Bora jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, Afisa Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Temeke, Michael Bachubila amesema taarifa za kuzuka kwa moto huo alizipata saa 11 alfajiri ambapo jitihada za uokoaji zilianza.
“Tulikuta moto umetanda eneo zima ambapo tumefanikiwa kuudhibiti kwa asilimia 90 na hakuna kilichookolewa katika godown hilo lenye vifaa vya ujenzi,”amesema.