Mgomo wa daladala katika Kituo cha Daladala Simu 2000 kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo umesitishwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, amesema amesikitishwa na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambao wametia dosari jina Halmashauri hiyo kwa uzembe na kutojua sheria.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Watendaji hao waliamua kuongeza ushuru kutoka Tsh. 500 hadi 1,000 bila kujua kuwa Sheria hairuhusu jambo Hilo.
Aidha, amesema kuwa wameagiza kurudi kiasi cha awali Tsh. 500 kwa siku kwa kila daladala na kuwa Baraza la Madiwani halikuongeza kiasi hicho kama inavyotakiwa na Sheria ambayo mabadiliko hayo kusainiwa na Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI, ndipo ianze kutumika lakini hakuna maombi ya namna hiyo yaliyotolewa na Baraza la Madiwani na hakuna Waziri aliyeruhusu jambo hilo.
Meya Jacob ameahidi hatua kali za kinidhamu kwa waliopandisha ushuru kinyume na Sheria inavyotaka, zitachukuliwa kwa waliohusika huku pia kero ndogo ndogo za stendi kama walinzi na wahudumu wa vyoo zitashughulikiwa.
ULIPITWA? Madereva wa daladala Kituo Cha Mawasiliano walivyogoma leo…tazama hapa chini!!!
Hali ya Ester Bulaya akiwa Hospital baada ya kuugua akiwa rumande…tazama hapa chini!!!