Kiungo wa zamani wa timu ya Taifa ya England na club ya Arsenal Jack Wilshere ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 30.
Wilshere ametangaza kustaafu na sasa inaelezwa kuwa atatangazwa kuwa kocha wa U-18 wa club ya Arsenal aliyoitumikia kwa muda mrefu.
Sio kawaida kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 30 kustaafu ila Wilshere amelazimika kufanya maamuzi magumu kutokana kiwango chake pia kuathiriwa na majeraha kiasi cha kukosa timu.
Wilshere amefanya maamuzi hayo baada ya kuachwa na club ya AGF Arhus akiwa kadumu na club hiyo kwa siku 136.