Mahakama kuu nchini Africa Kusini, imemhukumu kifungo cha Miezi 15 jela, aliyekuwa rais wa taifa hilo Jacob Zuma, baada ya kupatikana na hatia ya kukosa kuhudhuria vikao vya kamati iliokuwa inachunguza, tuhuma za rushwa dhidi yake
Hata hivyo jaji Sisi Khampepe, ambaye ametoa hukumu hiyo amesema, hukumu hiyo si ya lazima iwapo Zuma, atazingatia maagizo ya mahakama na kuanza kuhudhuria vikao vya kamati inayomchunguza.
Mwenyekiti wa kamati ya mahakama inayomchunguza Zuma, Raymond Zondo, alikuwa ameiomba mahakama kumfunga Zuma miaka miwili jela kwa kususia vikao vya kamati yake.
Tangu mwaka 2018, Zuma amekuwa akikabiliwa na kesi ya rushwa ambayo, amekuwa akikanusha kwa madai ya kuchochewa kisiasa.