March 7, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson kwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust alikabidhi msaada wa vitabu vya shule za msingi na sekondari za Wilaya ya Mbeya mjini vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 300 kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ikiwa ni kutimiza ahadi aliyoitoa mwezi February kwa lengo la kusaidia kukuza viwango vya ufaulu kwa wanafunzi mkoani humo.
Katika hotuba yake Dr Tulia alionyesha kutofurahishwa na maneno ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakisema kwamba hatimizi ahadi nyingine ambazo amekuwa akiziahidi kwa watu wake. “Tulia Trust imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa jamii ya watanzania lakini kumekuwa na baadhi ya maneno kwa watu kwamba tumekuwa hatutimizi ahadi zetu, wanachotakiwa kujua ni kwamba sisi huwa hatuahidi vitu ambavyo hatuna uhakika wa kuyatimiza” –Dr Tulia
Jafo ameongea juu ya kauli ya ‘Youtube’ maabara