Manchester United wanatarajia Jadon Sancho kuondoka katika klabu hiyo msimu wa joto bila kujali kama Erik ten Hag atasalia kuinoa au la, chanzo kilimwambia Rob Dawson wa ESPN.
Sancho alitolewa kwa mkopo kwa klabu ya zamani ya Borussia Dortmund mwezi Januari kufuatia kutofautiana hadharani na Ten Hag.
Mustakabali wa Mholanzi huyo kama meneja uko shakani baada ya msimu mbaya.
Sancho ana makubaliano na Dortmund hadi mwisho wa msimu, lakini bila chaguo au wajibu wowote kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu.
Timu hiyo ya Bundesliga ingependa kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, lakini vyanzo vimeiambia ESPN kwamba hawawezi kuendana na mshahara wake United na hawataweza kukidhi mahitaji yoyote ya ada kubwa.
Mkopo wa pili wa msimu wa 2024-25 unawezekana, lakini upendeleo wa United ni uhamisho wa kudumu.
Sancho, ambaye yuko chini ya kandarasi hadi 2026, alijiunga na United kwa mkataba wa pauni milioni 73 mwaka 2021 na klabu hiyo ingetaka kurejesha kiasi cha ada hiyo iwezekanavyo.
“Kwa hivyo tuseme hivi: [Jumatano dhidi ya PSG] alicheza vizuri sana na ni mchezaji mzuri sana,” Ten Hag aliambia mkutano wa wanahabari siku ya Alhamisi. “Jana alionyesha kwanini Manchester United walimnunua na alionyesha anawakilisha thamani kubwa kwa Manchester United, ambayo ni nzuri.
“Nina furaha kwa Jadon, kwa utendaji wake wa jana, na tutaona kitakachotokea siku zijazo.”