Kutokana na kero mbalimbali zinazolikumba soko la samaki feri Dar es salaam, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amefanya ziara leo May 8 2018 katika soko hilo na kujionea changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabishara hao.
Waziri Jafo baada ya kutembelea soko hilo na kuona hali ya soko, ametoa maagizo mbalimbali kwa Uongozi, mojawapo likiwa ni kutatua kero zote zilizotolewa na wafanyabishara hao na kurekebisha miundombinu ya soko hilo ndani ya siku 45.