Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, amewaagiza watendaji wa mikoa kuwatambua wamiliki wa majengo yanayotakiwa kulipiwa kodi ili wazilipe kama sheria ya ardhi inavyoelekeza.
Waziri Jafo ameyasema hayo hii wakati akiongea na maafisa wakuu wa wilaya, maafisa tarafa na wakurugenzi ambapo ametoa muda wa wiki tatu kwa zoezi hilo kukamilika na fedha zitakazokusanywa zinaingizwa moja kwa moja serikalini.
“Leo Februari 5 hadi tarehe 28, 2021, wiki hizi zote ziende zikatumike kwa ajili ya kwenda kubainisha majengo yote yaliyokuwa katika kila mtaa, tunataka tupate rekodi ya majengo yote ndani ya Tanzania ambayo yanakidhi kulipiwa kodi ya majengo kwa mujibu wa sheria”Waziri Jafo.
Baadhi ya watendaji wamesema katika zoezi hilo watazingatia miongozo ya serikali inavyoelekeza kuhusu ukusanyaji mapato ya serikali.