Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.
Katika ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.
Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama
Please see my Statement on failure to comply with court orders. pic.twitter.com/JvrXQB4mTd
— David Maraga (@dkmaraga) February 7, 2018
TOP 10: HIZI NDIZO HOTELI ZENYE VYUMBA VYA BEI ZA JUU ZAIDI DUNIANI