Taarifa iliyotolewa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa leo September 26 2016 imesema kuwa msimamo alioutoa msajili wa vyama vya siasa kuhusu mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF.
Taaarifa hiyo imesema kuwa kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa kwake na pande mbili zinazosiganana kwa mujibu wa katiba ya CUF toleo la 2014 msajili alijiridhisha kwamba, Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa Taifa wa chama cha CUF kwa sababu alitengua barua yake ya kujiuzulu kabla haijakubaliwa na mamlaka yake ya uteuzi kama inavyoelekeza ibara ya 117(2).
Aidha, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ina viasa vyombo vya habari kufanya jitihada za kuelewa msimamo wa msajili wa vyama vya siasa, badala ya kuandika habari au makala zinazopotosha umma.
Hivyo, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inatuma fursa hii pia, kukanusha taarifa zinazoenezwa katika vyombo vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii kwamba, msajili wa vyama vya siasa amesema kuwa hakumrudishia Profesa Lipumba uenyekiti wa Taifa wa CUF bali Profesa Lipumba kajirudisha mwenyewe kinyemela. Habari hiyo siyo ya kweli, imepotoshwa kwa makusudi, Watanzania wanapaswa kupuuzia.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inawaasa viongozi wa taifa wa chama cha CUF kusoma kwa makini msimamo uliowekwa na msajili wa vyama vya siasa na kuuheshimu kwani kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa sura ya 258, msajili wa vyama vya siasa anao wajibu wa kujiridhisha kwamba, mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika uongozi wa taifa wa chama cha siasa, ni halali na yamefanywa na mamlaka halali kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama husika.
ULIKOSA ALIYOYASEMA BAADA YA KUINGIA MAKAO MAKUU CUF? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI