Msanii wa muziki wa hip-hop Drake ametupiliwa mbali na kesi yake kuhusu tamasha baya la Astroworld 2021 huko Houston ambapo watu 10 waliuawa, kulingana na jaji .
Drake alikuwa mgeni maalum wa mkali wa rap Travis Scott katika show yake, ambaye alikuwa ameongoza tamasha hilo.
Alitumbuiza na Scott mwishoni mwa tamasha hilo Novemba 5, 2021, umati ulipoongezeka na waliohudhuria walikuwa wamejaa sana hivi kwamba wengi hawakuweza kupumua au kusogeza mikono au miguu yao. Mamlaka na waandalizi wa tamasha walikuwa wakijaribu kuzima onyesho lakini bado lilileta maafa.
Familia za watu 10 waliofariki wakati wa tamasha hilo, pamoja na mamia ya waliojeruhiwa, waliwashtaki Drake, Scott na Live Nation – promota wa tamasha hilo – pamoja na makumi ya watu wengine na mashirika.
Wengi wa wale ambao walishtakiwa, ikiwa ni pamoja na Drake na Scott, wamemwomba Jaji wa Wilaya Kristen Hawkins kufuta kesi dhidi yao. Siku ya Jumatano, Hawkins alimfukuza Drake katika kesi hiyo kwa utaratibu mfupi.
Mawakili wa Drake, ambaye jina lake kamili ni Aubrey Drake Graham, walikuwa wamejitetea wakati wa kusikilizwa kwa mahakama Aprili 1 huko Houston kwamba hakuhusika katika kuandaa tamasha hilo hivyo hahusiki kwa vifo na majeruhi yaliyotokea.