Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro Mheshimiwa Paul Ngwembe amewataka wadau wa haki jinai kuharakisha upelelezi wa mashauri ili kutoa fursa kwa Mahakama kutenda haki kwa wakati.
Jaji Ngwembe ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wadau wa haki jinai kutoka Jeshi la Polisi, TAKUKURU ,Ofisi ya Mashitaka,mamlaka za Dawa kulevya ,mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori na Ofisi ya kudhibiti fedha haramu.
Mh. Ngwembe amesema zipo baadhi ya taasisi uchelewesha upelelezi Mashauri jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa mlundikano wa mahabusu kukaa muda mrefu bila sababu za msingi.
Anasema Mashauri ambayo upelelezi wake huchelewa ni pamoja na mauaji na ubakaji na kusababisha Watuhumiwa kukaa muda mrefu mahabusu bila kupata haki Yao hivyo Mashauri hayo yanaweza kukamilika ndani ya siku tisini tuu endapo wadau wote watatimiza wajibu wao.
Ngwembe anasema mashauri ya Jinai Upelelezi wake unaendeshwa kisayansi zaidi hivyo jamii utambue kua Mahakama lazima ipate ushahidi wa uhakika ndipo itoe hukumu hivyo wananchi waendelee kuziamini Mahakama.
Pamoja na hayo jaji Ngwembe amezungumzia suala la utolewaji nakala za hukumu ambapo zinapaswa kutolewa mara tu ya hukumu kutolewa ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kikata Rufaa endapo hawajaridhika na maamuzi.
Kwa upande wake Naibu msajili Mwandamizi mahakama kuu Bwana Arnold John Kirekiano amesema mafunzo hayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na chuo cha Uongozi wa mahakama Lushoto Kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitoa mradi wa maboresho awamu ya pili.
Lengo la Mafunzo hayo ni kupunguza na kumalzia mashauri ya mlundikano yalipo Mahakamani yanayochelewa kusikilizwa kutokana na Upelelezi kutokakamilika kwa wakati ifikapo mwaka 2025.