Jaji Mfawidhi wa Mhakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro,Mh.Latifa Mansoor ameushauri Uongozi wa Shrika la Wasaidizi wa Kisheria Morogoro (MPLC) kuongeza nguvu katika kutoa elimu na msaada wa Kisheria ndani ya jamii kwa lengo la kupanua wigo wa upatikanaji wa haki ili kupunguza matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo ukatili wa kijinsia,ubakaji,ulawiti na maadili.
Aidha Jaji Mfawidhi, Mh Latifa Mansoor ametoa wito kwa mashirika yanajihusisha na utoaji huduma ya msaada wa kisheria kuongeza nguvu katika kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu nchini ili kusaidia kupunguza msongamano wa wafungwa.
Jaji Mfawidhi,Mh.Latifa Mansoor ametoa rai hiyo wakatika uongozi wa shirika la Wasaidizi wa Kisheria Morogoro (MPLC),ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Amani Mwaipaja walipomtembelea Mh.Jaji Latifa, kwa lengo la kujitambulisha na kuongeza wigo utendaji katika upatikanaji haki.
Mkurugenzi Mtendaji wa MPLC,Amani Mwaipaja amempongeza Jaji kwa kazi anazofanya,na kupokea ushauri uliotolewa kwa lengo la kuhakikisha jamii inapata haki.
Mwaipaja anasema katika kufikia jamii kwa wingi shirika la MPLC limeandaa Jukwaa la MPLC ambalo litafanyika mjni Morogoro mnamo 28/6/2024 Lengo la jukwa ni kukutanisha wadau mbalimbai, fursa ya kutoa elimu, kujadili na kujifunza mbinu mbalimbali za utatuzi wa migogoro inayowakabili wananchi ndani ya jamii ikiwemo masuala ya ardhi,ukatili wa kijinsia,ulawiti na matunzo ya watoto.
Pia anasema katika jukwaa hilo litatoa fursa kwa wenye changamoto mbalimbali kujifunza, kupata ushauri, mwongozo na msaada wa kisheria bure,hivyo wananchi kujitokeza kupata elimu na ushauri katika mashauri yanayowatatiza.