Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga ameeleza kuwa atamshauri Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuvunja bunge la nchi hiyo baada ya kushindwa kupitisha sheria inayowatambua watu wanaozaliwa na jinsia mbili.
CJ Marag katika hatua yake ambayo haijawahi kutokea hapo awali, amesema kwamba bunge limekataa kufuata agizo la Mahakama Kuu la kutunga sheria inayotambua watu wenye jinsia mbili kwa zaidi ya miaka 9.
“Haiwezekani kwamba Bunge alijatii agizo la Mahakama kuu katika maombi ya kikatiba No. 371 ya 2016 kwa zaidi ya miaka 9 sasa bunge halijatunga sheria inayohitajika kutekeleza sheria ya jinsia mbili ambayo, kama korti ya rufani ilivyozingatia katika uamuzi wake ni dhahiri bunge halijali mtazamo kuhusu jambo hili,”.
“Ikiwa Bunge litashindwa kutunga sheria kwa mujibu wa agizo chini ya kifungu cha (6) (b), Jaji mkuu atamshauri Rais atavunja bunge, ni jukumu langu kikatiba kukushauri Rais wa Jamuhuri ya Kenya” Jaji Maraga
RAIS MAGUFULI “VITAMBULISHO VYA MACHINGA HAVILAZIMISWI”