Katika kusheherekea hatua muhimu ya Kampuni ya Heineken kununua Kampuni ya Distell Group Holding Limited (Distell) na Namibia Breweries Limited inatarajia kuzindua Jalada lake jipya la bidhaa jumamosi ya Mei 25, 2024 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saam Mei 22, 2024, Meneja Mkazi hapa nchini wa kampuni ya HEINEKEN, Obabiyi Fagade, amesema kuwa kampuni hiyo imeshakamilisha Manunuzi ya Kampuni ya Distell Group Holdings Limited (‘ Distell’) na Namibia Breweries Limited (‘NBL’).
Katika Sherehe hiyo itakyofanyika Mei 25, 2024 Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ambapo atajumuika na wadau wengine mashuhuri na viongozi wa tasnia mbalimbali.