Leo May 23, 2018 Askofu Mkuu wa kanisa katoliki nchini Australia, Adelaide Philip Wilson amejiuzulu nafasi yake ya uongozi wa juu wa kanisa hilo baada ya kukutwa na hatia ya kuficha uovu uliotendwa na Padri mwezake Fletcher wa kulawiti.
Askofu huyo mwenye miaka 67 anakabiliwa na kifungo cha miaka 2 jela kwa kosa hilo la kufumbia macho na kushindwa kutoa ripoti kwa mamlaka husika juu ya kitendo hicho ambacho ni kinyume na sheria za nchini humo alichokifanya Padre James Fletcher cha kulawiti watoto wanaotumikia kanisani kwenye miaka 1970.
Wilson ambaye ndiye Askofu mwenye nafasi juu ya uongozi wa kanisa Katoliki Australia amesema anaachia madaraka yake ya uongozi wa kanisa hilo na yuko tayari hata kujiuzulu uaskofu wake ikimbidi kufanya hivyo.
Askofu Wilson alikuwa Padre tu wakati Padre Fletcher akifanya maovu hayo na Padre Fletcher alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela ambapo mwaka 2006 alifariki gerezani ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya hukumu.
Mkuu wa Wilaya atoa machozi ‘kwa kipigo walichopata Wananchi wake’