Mtu mmoja asiyefahamika jina wala anakotokea wapi anayedhaniwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi katika majibizano ya risasi kati ya Maaskari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na majambazi watano waliokuwa wamejihami kwa silaha katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha jijini Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jerome Ngowi, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kumamkia juzi saa 6:10 usiku baada ya wananchi kutoa taarifa za siri kuhusu watu hao.
Amesema baada ya Jeshi hilo kupata taarifa hizo lilituma kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu ambacho baada ya kufika katika eneo hilo wahalifu hao walishtuka kuwa wanafuatiliwa na ndipo wakaanza kutimua mbio.