Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh Judith Nguli ameiagiza Kamati ya afya Wilayani humo kuhakikisha inaweka Mpango mkakati wa kutoka elimu kwa umma dhidi ya magonjwa ya Mlipuko pamoja na ugonjwa wa Usubi
Hayo yamebainishwa alipokuwa akizungumza na kamati hiyo kwenye kikao maalumu chenye lengo la kuangalia tathimini ya kujikinga na magonjwa yasiyopewa kipaumbele kilichofanyika Wilayani hapo
Aidha amesema kuwa uwepo wa Imani potofu umekuwa chanzo cha kutotilia mkazo juu ya magonjwa mengine hatarishi kama Usubi hivyo kamati ya afya ameiagizwa kuhakikisha inaenda kutoa elimu kwa jamii jinsi na namna ya kujikinga na ugonjwa
Kwa Upande wake Mganga mkuu Wilayani humo Dkt Phillipina Phillipo amesema kuwa uwepo wa magonjwa ya mlipuko umekuwa tishio kubwa ndani ya Mkoa wa Morogoro hivyo kamati ya afya itaenda kuangalia namna ya kupambana na magonjwa kama kipindupindu yasipate nafasi ndani ya Wilaya ya Mvomero
Wakitoa hoja zitakozenda kusaidia juu ya Kupambana na mlipuko wa magonjwa haya wamesema wataenda msako wa kushtukiza kwenye Baaadhi ya maeneo kama sehemu za starehe migahawa ya Mama lishe jli kuona hali ilivyo na badaye kutoa elimu kwao dhidi ya magonjwa hayo