Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Wataalamu wanaharibu, Wanasiasa wananyamaza kimya. Nchi haisongi. Tunahitaji kuwajibishana. Kwa nyakati hizi, tunahitaji Rais muwajibishaji!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 16, 2015
Tanzania baada ya JK, inahitaji Rais atakayekimbiza maendeleo, atakayetoa motisha ya watu kufanya kazi, ubunifu, atakayewajibisha wazembe! — Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 16, 2015
Hospitali ya wilaya ya Kilwa. Hali yake ni pathetic. Vyoo vya wodini vibaya na vichafu kuliko jela! Makorido rafu. Maji after evry 5 days!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) January 16, 2015
Facebook:
CLoudsFM: WANNE WAFA AJALINI,PWANI
WATU wanne wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Abiria la Hajees likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam na lori katika eneo la Mandera Mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei amesema kuwa abiria hao waliruka kutoka katika basi hilo kuhofia ajali ya kugongana na lori lililokuwa likitokea mbele ya basi hilo na ndipo walipoangukia barabarani na kupelekea vifo vyao, baada ya dereva wa basi kutoka nje ya barabara.
Aidha Kamanda Matei amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wa Chanzo cha ajali hiyo wanamshikilia dereva wa lori hilo ambalo lilisababisha vifo vya abiria hao walioruka kutoka katika basi la Hajees
Blogs
Saleh Jembe
VURUGU TAIFA CUP MWAMUZI, KIONGOZI AFUNGIWA, MMOJA ASIMAMISHWA
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Januari 15 mwaka huu) kupitia ripoti ya mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza kati ya Shinyanga na Simiyu ambayo ilivunjwa na mwamuzi katika daika ya 70.
Baada ya kupitia ripoti, Kamati imebaini kuwa licha ya vurugu alizofanyiwa mwamuzi, bado mechi hiyo ingeweza kuendelea kwa kuchezeshwa na mwamuzi wa akiba kwa vile usalama ulikuwepo baada ya yeye kupigwa.
Pia Kamati imeagiza Katiba wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Sologo aliyeripotiwa kumpiga mwamuzi suala lake lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi, wakati Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye naye alishiriki kumpiga mwamuzi amesimamishwa wakati akisubiri kuchukua hatua zaidi.
Kamishna wa mechi hiyo Idd Mbwana, na mwamuzi Joseph Pombe wamefungiwa kwa miaka miwili.
Mechi kati ya Shinyanga na Simiyu itamaliziwa dakika kumi zilizobaki kesho (Januari 17 mwaka huu) mjini Shinyanga. Kila chama cha mkoa kitabeba gharama zake katika uendeshaji wa mechi hiyo ambayo mwenyeji ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA).
Timu itakayosonga mbele baada ya mechi hiyo itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili ugenini Januari 19 mwaka huu dhidi ya Kigoma. Mechi za marudiano za raundi ya pili zitachezwa kati ya Januari 21 na 22 mwaka huu.
Hatua ya robo fainali hadi fainali ambayo mechi zake zitachezewa jijini Dar es Salaam itaanza Januari 26 mwaka huu. Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu.
Vilevile Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imemfungia kwa miaka miwili Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda kwa kushindwa kuingiza timu yake uwanjani kwenye mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza dhidi ya Dodoma iliyokuwa ichezwe kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
PLUIJM AAMUA KUMBANDIKA COUTINHO JINA LA UTANI, SASA AMUITA ROMARIO
Bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Han van Der Pluijm, amembadilishia jina kiungo wake mshambuliaji, Andrey Coutinho na sasa anamuita Romario de Souza Faria.
Romario ni straika wa zamani wa Brazil aliyetamba miaka ya 1990 mpaka 2000, hasa kwenye kikosi cha taifa cha Brazil.
Kocha huyo raia wa Uholanzi, alianza kusikika akimfananisha Coutinho na Mbrazili mwenzake huyo katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo Ununio jijini Dar es Salaam, juzi.
Pluijm alikuwa akimuita Coutinho kwa jina hilo la Romario kila alipokuwa akitaka kutoa maelekezo kwake na kiungo huyo hakusita kuitikia.
Alipoulizwa kocha huyo sababu ya kumuita jina la Romario alifunguka: “Sitamuita jina la Coutinho tena, sasa nitamuita Romario kutokana na aina yake ya uchezaji kufanana na Romario.”
BBC Swahili:Amavubi kutua Mwanza January 21
Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) itawasili Mwanza, Tanzania Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.
Baada ya kocha Mdachi, Mart Nooij kutaja kikosi, Stars inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.
Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.
Mwananchi:
Sakata la Escrow: Vigogo wa BoT, TRA, Tanesco wapandishwa kizimbani
Dar es Salaam. Meneja Misamaha ya Kodi TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa , Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na Mkurugenzi wa fedha BOT , Julius Rutta Angello wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
Watuhumiwa hao wanafanya idadi ya waliofikishwa mahakamani kwa kashfa ya miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow kufikia watano baada ya watumishi wengine wawili wa umma kufikishwa mahakamani hapo Jumatano iliyopita.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliwekewa kiasi cha Sh323 milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001.
Mwingine ni Mhandisi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (Rea), Wizara ya Nishati na Madini, Theophillo Bwakea aliyepokea rushwa ya Sh161,700,000 kupitia akaunti yake namba 004101102643901.Mahakama ya Kisutu leo
Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2015, walifikishwa kwa mahakimu wawili tofauti, Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda na Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka.
Akisoma hati ya mashtaka katika kesi namba 16 ya 2015 inayomkabili Kyabukoba, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai mbele ya Hakimu Kaluyenda kuwa Januari 27, 2014 katika Benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala , alipokea Sh1.6 bilioni kupitia akaunti namba 00110202613801.
Swai alidai kuwa mshtakiwa huyo akiwa katika Benki ya Mkombozi alijipatia kiasi hicho cha fedha ambacho ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow na kwamba alizipokea kutoka kwa James Burchard Rugemalira ambaye ni Mshauri huru wa Kitaalam, Mkurugenzi wa VIP Engineering na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits ambayo ni mali ya Rugemalira mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria.
Alidai kuwa Julai 15, 2015, mshtakiwa huyo Kyabukoba akiwa katika benki hiyo ya Mkombozi alipokea rushwa ya Sh161.7 milioni, Agosti 26,2014 alipokea tena rushwa ya Sh 161.7 milioni na Novemba 14, 2014 alijipatia rushwa ya kiasi kingine cha fedha cha Sh161.7 milioni kupitia kwenye akaunti hiyo, kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni hiyo ya Rugemalira mahakamani kitu ambacho ni kinyume cha sheria na kwamba fedha zote hizo ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Kyabukoba aliyakana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo umekwisha kamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali (PH).
Tatizo hutokea mhusika akiwa usingizi,hivyo hushindwa kujizuia
Kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kukojoa kitandani au kujikojolea ni jambo la kawaida. Lakini vijana na watu wazima kujikojolea kitandani mara kwa mara siyo jambo la kawaida katika jamii. Watu wenye tatizo hili hujulikana kama vikojozi.
Kitabu cha afya ya akili kilichotolewa na Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Akili cha Marekani kinasema kwamba kikojozi ni mtu mwenye tatizo la kujikojolea nguoni au kitandani angalau mara mbili ndani ya kipindi cha wiki moja na kwa muda wa miezi mitatu mfululizo akiwa na umri wa miaka mitano au zaidi. Katika tafiti mbili zilizochapishwa mwaka 2003 kuhusu ukubwa wa tatizo la watoto vikojozi, ilibainika kuwa idadi yao ni kubwa katika jamii kufikia kati ya asilimia 14.7 na 20.
Tafiti kadhaa za afya ya jamii zinabainisha kuwa watoto wa kiume hukabiliwa zaidi na tatizo hili kuliko wa kike kwa uwiano wa 2:1.
Pia utafiti mwingine unaonyesha kuwa watoto wa kiume wanakabiliwa na tatizo hili mara tatu zaidi ya watoto wa kike. Katika utafiti uliochapishwa Septemba 2014 katika jarida la kisayansi la IOSR Journal of Dental and Medical Sciences, Dk A.R.C Nwokocha na wenzake wa Chuo Kikuu cha Nigeria walibaini kuwa asilimia 15.82 ya vijana walioko shule za sekondari nchini humo ni vikojozi.
Takwimu nyingine zinaonyesha kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi.
Kwa maana hiyo nchi ikiwa na idadi ya watu milioni 50 kama Tanzania, basi idadi ya watu wazima vikojozi inakadiriwa kuwa ni sawa na nusu milioni.
Ingawa tatizo la kujikojolea linaweza kutokea wakati wa mchana, ushahidi mwingi unaonyesha kuwa tatizo hili hutokea mara nyingi zaidi usiku wakati mhusika anapokuwa usingizini.
Hali hii inapomtokea mtoto au mtu mzima, anakuwa hajielewi na ni jambo linalokuwa nje ya uwezo wake katika kujitawala.
Wanasayansi wanatoa sababu nyingi zinazofanya watoto kuwa vikojozi.
Katika utafiti wao Gulnaz Culhal na Nizami Duran wa Chuo Kikuu cha Mustafa Kemal cha nchini Uturuki, walibaini kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ya minyoo aina ya enterobius vermicularis na tatizo la watoto kukojoa kitandani usiku.
Watoto wenye aina hii ya minyoo walikabiliwa na tatizo la kukojoa kitandani kwa asilimia 51.3 na walipotibiwa, tatizo lilipungua hadi kufikia kiasi cha asilimia 28.8.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la European Journal of General Medicine toleo la 3 (1) la mwaka 2006.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook