Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amesema kuanzia January hadi November 2021 ni Wananchi 12 wamejinyonga katika Wilaya hiyo kutokana na wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi na ugumu wa maisha.
Kanoni amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama mbele ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Eng. Marwa Rubirya wilayani hapo.
Baadhi ya Wananchi wamesema ili kutokomeza tatizo la Watu kujinyonga Serikali inatakiwa kuweka Washauri wa umri tofauti pamoja na Vipngozi wa Serikali za vijiji kumaliza tofauti za wenye malalamiko kwa wakati bila kuchelewesha na kupendelea upande mmoja.