Ni miezi miwili tangu nchi ya Japan ikumbwe na matetemeko mawili ya ardhi yaliyopelekea zaidi ya watu 50 kupoteza maisha na maelfu kujeruhiwa katika mji wa Kumamoto nchini humo. Tangu matetemeko hayo yatokee ni zaidi ya watu 200 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa tetemeko la ardhi.
Wagonjwa hao hupata kizunguzungu, kichefuchefu na kukosa nguvu, pia inasemekana bado wanapata hisia za hofu na wasiwasi juu ya maisha yao na wakihisi kuna uwezekano tetemeko lingine linaweza kutokea na kuhatarisha maisha yao. Hali hii wameiita ‘jishin-yoi’ ikiwa ina maanisha ‘ulevi wa tetemeko la ardhi’.
Matetemeko hayo mawili yalipelekea zaidi ya nyumba 410,000 kubaki bila maji na nyingine 200,000 bila umeme hali iliyosababisha watu wengi kukaa katika foleni kwa ajili ya chakula na maji katika vituo vya misaada ya dharura, Japan imekua ikikumbwa na matukio ya namna hii mara kwa mara.
VIDEO TETEMEKO HILO LILIVYOSABABISHA MAAFA JAPAN>>
ULIIKOSA HII YA TAARIFA ZA KUGUNDULIKA KWA GESI MPYA TANZANIA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE