Baada ya nchi ya Kenya kutaja mipango yake ya kurudisha wananchi wake kutoka nchini Sudan siku ya jana hii leo pia Japan pia imetangaza siku ya leo Jumatano Aprili 19, 2023 kuwa inajiandaa kuwandoa raia wake nchini Sudan, na kuwa nchi ya kwanza kuchukua hatua hiyo nchini humo ambako ghasia zimekuwa zikiendelea tangu Jumamosi licha ya wito wa kusitisha mapigano.
Takriban raia 60 wa Japan wako nchini Sudan, wakiwemo wafanyakazi wa ubalozi, msemaji wa serikali Hirokazu Matsuno amesema Jumatano.
Wizara ya Ulinzi imefanya “maandalizi ya lazima” kwa ajili ya zoezi hilo la kuwaondoa raia wa Japan nchini Sudan, amesema katika mkutano na waandishi wa habari, akihakikisha kwamba serikali inafanya “kila iliwezalo kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa Japan.”
Mapigano nchini Susan kati ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Jenerali Mohammed Hamdan Dogolo (RSF) na jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, malakani tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, tayari yamesababisha vifo vya karibu watu 200. tangu Jumamosi kulingana na Umoja wa Mataifa.