Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya ukaguzi kwa Wafanyabiashara kuhusu matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Efd, ambapo mchakato huo umefanyika majira ya usiku kuanzia saa 4 hadi saa 6 maeneo ya Kinondoni na Sinza Dar es Salaam.
Akizungumza na Ayo Tv na millardayo.com, Meneja Msaidizi wa Madeni wa TRA Kinondoni, Sylver Rutagwelera amesema zoezi hilo ni endelevu lenye lengo la kutoa elimu kupitia mashine hizo.
“Zoezi hili tunafanya mchana na usiku kama unavyoona muda huu saa 6 usiku tunafanya kazi ili kuhakikisha wafanyabiashara wa mkoa wa Kinondoni wenye mauzo kuanzia Milioni 14 na kuendelea wananunua mashine za Efd,”amesema
Amesema licha ya kutoa elimu wapo wafanyabiashara bado ni wakahidi, hivyo wataendelea kutoa elimu na wale watakaokwenda kinyume watawachukulia hatua.