Ikiwa ni siku ya pili tangu kuzinduliwa kwa mashindano ya ngoma za asili ya Tulia Traditional Dances Festival 2018 ambayo muhasisi wake ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ambayo yanafanyika Wilayani Rungwe mkoani Mbeya yakishirikisha makundi ya ngoma nchi nzima, Dr. Tulia ameahidi kuanzisha kituo kikubwa cha utamaduni nchini huku akiwataka watu kuacha kulalamika kwamba hakuna ajira na badala yake wazitumie vizuri fursa zinazowazunguka.
Waziri Mwakyembe na Dr. Tulia walivyosakata rumba mbele ya watu wao Mbeya