Siku ya January 21 2016 haiwezi kuwa nzuri kwa kiungo mkabaji na beki wa kati wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Javier Mascherano, ameingia kwenye headlines baada ya January 21 kuenea kwa taarifa za kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.
Javier Mascherano amehukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja na faini ya pound 625000/=, baada ya kukutwa na hatia ya makosa mawili ya ukwepaji kodi. Javier Mascherano amehukumiwa kifungo cha miezi minne na kifungo cha miezi nane kwa kosa la ukwepaji kodi mwaka 2011 na 2012, miezi ambayo ukijumlisha kwa pamoja ndio inakuwa mwaka mmoja.
Hata hivyo mwanasheria wa staa huyo David Aineto ameomba iondolewe adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela na apigwe faini, kitu ambacho Javier Mascherano anaweza kulipa. Nchini Hispania sheria ya mtu akihukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili ana nafasi ya kuomba adhabu yake ibadilike kutoka kifungo kuwa faini, kama tu kosa lake likiwa sio la jinai.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.