Utafiti uliofanywa siku za hivi karibuni na Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) Marekani umeeleza kuwa taarifa za uongo duniani husambaa mara sita haraka zaidi na kuwafikia watu kwenye mtandao wa Twitter kuliko taarifa za ukweli.
Inaelezwa kuwa utafiti huu ni wa kina zaidi kuwahi kufanyika juu ya ongezeko la kusambaa kwa habari zisizo za kweli kwenye mitandao ya kijamii.
Utafiti huu ulifanywa kwa kuangalia habari 126,000 ambazo ziliwekwa kwenye mtandao wa Twitter katika kipindi cha miaka kumi ambacho ni kati ya 2006 na 2016 ili kuona kama habari hizo zilikuwa sahihi au la.
Watafiti walibaini kuwa kwa wastani habari za uongo zilisambaa na kuwafikia watumiaji wa mtandao huo wa Twitter 1,500 ndani ya masaa 10, hii ikionesha kuwa habari za uongo zilifikia asilimia 35 zaidi kwa watu.
Habari za ukweli zilipostiwa tena ‘retweet‘ lakini asilimia 1 tu ya habari za uongo zilifikia watu 100,000, na kwa ujumla habari za uzushi zilikuwa na uwezekano wa kupostiwa tena kwa asilimia 70.
Polisi makao Makuu wamezungumzia matukio ya mauaji ya hivi karibuni