Leo January 23, 2018 Kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga ya tuhuma za kutoa lugha ya fedheha dhidi Rais John Magufuli imeahirishwa baada ya kutokea mabishano ya kisheria.
Katika usikilizwaji wa kesi hiyo, Wakili Mkuu wa Serikali Joseph Pande ameiomba Mahakama isikilize video na sauti za watuhumiwa walipokuwa wakihutubia December 30 2017.
Leo January 23, 2018 shahidi wa nne upande wa Serikali Sajenti Daniel Masanja ameiambia Mahakama kuwa alipokea tape recorder kutoka kwa Inspector Joram Magova ambaye ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Mbeya December 30, 2017.
Sajenti Daniel amesema alipokea recoder hiyo na kuisajili katika kitabu cha kumbukumbu. January 2, 2018 aliombwa na Inspector Joram kwa ajili ya kuwasikilizisha watuhumiwa Mbunge Joseph Mbilinyi na Katibu Masoga katika chumba cha mikutano katika ofisi ya Kamanda wa Polisi.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi Boniphace Mwabukusi na Hekima Mwasipu waliiomba Mahakama kutopokea vielelezo hivyo kwa kuwa mashahidi hawakuwepo eneo la tukio na recorder hiyo inaweza kuchezewa.
Hakimu Michael Mteite aliahirisha kwa muda shauri hilo ambapo baada ya muda alitoa uamuzi wa kupokelewa vielelezo hivyo na kuwa kielelezo cha pili.
Inspector Joram Magova ambaye ni shahidi wa pili ameiambia Mahakama kuwa alifika eneo la mkutano na kusikiliza mkutano huo ambapo aliyeanza kuzungumza alikuwa ni Katibu Masonga, baadaye Katibu alimkaribisha Mbunge Joseph Mbilinyi ambaye alianza kuelezea shughuli za maendeleo na baadae alikazia maneno ya Katibu wake kumfedhesha Rais John Magufuli.
Wakili wa Serikali Joseph Pande aliiomba mahakama isikilize sauti hizo za watuhumiwa zilizorekodiwa na Inspector Magova ndani ya mahakama. Hoja hiyo ilipingwa na Wakili Mwabukusi akinukuu kifungu cha sheria ya mitandao namba 18 (3)(b) ya mwaka 2015 na 18 (2)(a)(b) ya mwaka 2015.
Baada ya mabishano ya kisheria ya Mawakili hao Hakimu Michael Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24 mwaka huu atakapotoa uamuzi wa sauti isikilizwe au la. Watuhumiwa wamerudishwa mahabusu.
VIDEO: “NABII TITO” AMWAMBIA KAMANDA “MIMI NINATUMIA BIBLIA”