Kutokana na kuharibika kwa Miundombinu ya reli maeneo ya Munisigala Kilosa Morogoro, January 25, 2018 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Eng. Atashasta Nditiye amefanya ziara katika maeneo hayo na kutoa maagizo.
Eng. Nditiye amewataka wananchi wanaoendesha shughuli za kilimo katika eneo hilo kuhama ndani ya miezi sita kwa sababu zinachangia uharibifu miundombinu hiyo ya reli. Pia amepongeza utendaji kazi wa kasi unaofanywa na wafanyakazi wanaokarabati reli hiyo.
WAZIRI MWIGULU ASIMAMISHA ZOEZI LA UTOAJI WA HATI ZA KUSAFIRIA (PASSPORT)