Waziri wa Usalama wa Argentina, Patricia Bullrich, anatumai winga Angel Di Maria atarejea nchini kuichezea Rosario Central.
Tangu Di Maria apokee tishio katika nyumba ya familia yake nje kidogo ya jiji la Rosario mapema mwaka huu, kiungo huyo wa kati wa Benfica amesema hatarejea kumalizia soka lake nchini Argentina. Watu watatu walikamatwa kuhusiana na vitisho hivyo mwezi Machi.
Bullrich alisema: “Jiji la Rosario linapitia hali ya kawaida. Natumai tunaweza kutuma ujumbe huo na kwamba angel Di Maria atarejea.
Nilizungumza na baba yake mara mbili au tatu.
“Waliogopa sana na ninawaelewa. Wao (mafia) huchagua watu maarufu lakini familia yake (Di Maria) inaishi huko.
Ilileta mshtuko, hiyo ndiyo ninaiita narcoterrorism. Inazalisha hali ya hofu na Di Maria alifikiria upya uamuzi wake. Ni uamuzi wa kibinafsi na wa familia.”
Di Maria, 36, anakuwa mchezaji huru msimu huu wa joto na bado hajatangaza klabu yake ijayo baada ya kazi ambayo ameichezea Real Madrid, Man United, PSG na Juventus.