Tarehe 5 kama ulikuwa hufahamu basi ni siku ya kimataifa ya upokonyaji silaha na kuzuia uenezaji wa silaha duniani na iliadhimishwa jana tarehe 5 Machi ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya umoja wa mataifa.
Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alibainisha kuwa matumizi ya kijeshi yanaendelea kuvunja rekodi, takwimu zinaonyesha kuwa watu 26,000 wanaweza kutibiwa malaria kwa gharama ya kununua kifaru kimoja cha kivita.
Antonio Guterres amesema siku hii ililenga na inalenga kukuza ufahamu na uelewa wa masuala ya upokonyaji silaha, hasa miongoni mwa vijana.
Azimio la kuunda siku hii lilipitishwa mwezi Desemba 2022, na kuthibitisha jukumu la Umoja wa Mataifa katika upokonyaji silaha na ahadi kwa nchi wanachama kuimarisha kanuni hii.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa, silaha hizi na zingine zinaendelea kutishia maisha ya mwanadamu na viwango vya rekodi ya hali ya juu ya matumizi ya kijeshi.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa mwaka 2021, matumizi ya kijeshi duniani yalifikia gharama ya dola trilioni 2.1.