Usalama wa mtandao ni utumiaji wa mtandao unao fuata kanuni, sheria na tahadhari ili kujihakikishia usalama katika matumizi yako ya mtandao ambapo hatua hizi husaidia katika ulinzi wa taarifa zako binafsi zidi ya hatari zinazoletwa na matumizi teknolojia na intaneti na atari hizo hufaamika kama uhalifu wa mtandaoni ‘Cybercrime’.
Elimu ya usalama mtandao inasaidia kupunguza athari za uhalifu mtandao ambazo husababishwa na udhaifu wa mwanadamu.
Hivyo, programu ya elimu kwa umma ya matumizi salama ya mtandao ni dhana muhimu inayoongeza ujuzi na maarifa kwa watendaji na kuwawezesha kubaini viashiria vya mashambulizi kabla ya kusababisha madhara kwa mwananchi, taasisi na nchi kwa ujumla.
Kwa kulijua hili shirika la Zaina Foundation limetoa elimu kwa taasisi mbalimbali nchini pamoja na waandishi wa habari juu ya usalama wa matumizi ya mtandao ya mara kwa mara na kuonesha ni kuwa ni muhimu kwa biashara ,mtu binafsi au taasisi hususan kwa namna gani inazuia changamoto kadhaa kama vile upotevu wa fedha, upotevu wa haki miliki, uharibifu wa taswira ya taasisi/biashara, upotevu wa wateja, n.k.
Moja ya maeneo muhimu ya kuangazia ni pamoja na :
Programu za simu – Programu nyingi huhitaji kujaza taarifa zako ili uweze kutumia. Pia programu nyingine huunganishwa na program nyingine kupata taarifa zako mbalimbali hivyo kuwa salama unahitaji kupakua program kutoka kwa mtengenezaji anayetambulika.
Jambo la pili Linki za kuingia tovuti mbalimbali- muhimu ni kuhakiki jina sahihi la tovuti ‘domain name’. Kwani wahalifu wengi hubadili jina halisi na kuweka tofauti ndogo ambayo sio rahisi kugundulika ;Mkurugenzi wa Zaina Foundation
Zaituni Njovu mkurugenzi Zaina Foundation amesema kuwa usalama wa mtandao ni muhimu kwa sababu hulinda watu binafsi na mashirika dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni na wizi au upotevu wa taarifa nyeti na za siri.
Usalama wa mtandao unaweza kufuatilia mifumo ya kulinda data ya kibinafsi (PII, PHI, maelezo ya kifedha n.k.), siri za biashara, mali miliki na taarifa zozote nyeti za serikali
Hakikisha unafungua linki yenye https mwishoni kuashiria usalama wako. Na sio yenye http maana taarifa zako zitakua wazi.
Huu ni Mchezo wa kuzima Mtandao iliyoundwa kwa lengo la kusaidia kuandaa shughuli ya mafunzo ya kushirikisha na ya kuelimisha ambayo inatoa mwanga juu ya mbinu mbalimbali za kuzimwa kwa mtandao na njia za kuzikabili.