Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, amefariki Dunia katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es salaam, ambako alikuwa akipatiwa matibabu na maziko yake yanatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni Zanzibar.
Akiwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha atakumbukwa kwa maamuzi ya kufuta Matokeo ya Uchaguzi Zanzibar mwaka 2015 akidai Uchaguzi huo haukuwa huru na gaki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa Sheria za Uchaguzi.
Mkurugenzi wa sasa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Thabit Idarous Faina amethibitisha kifo cha Jecha ambapo amesema “”Ni kweli Jecha amefariki dunia na tunasubiri mwili wa marehemu kutoka Dar es salaam na kuwasilishwa hapa Unguja kwa ajili ya mazishi leo saa 10 jioni”