Baada ya Simba kuendelea na malalamiko ya muda mrefu kuwa klabu ya Dar Es Salaam Young African inapendelewa na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa mambo kadhaa, ikiwemo wachezaji na viongozi wake kutopewa adhabu. Mchana wa March 16 mkuu wa idara ya habari wa Yanga Jerry Muro ameweka wazi suala hilo.
Jerry amelazimika kuweka wazi kwa wanaosema kuwa yeye amemkosea msemaji wa Simba na anatakiwa kuadhibiwa, wanakosea kwani kama angekuwa amekosea angeshitakiwa katika vituo vya polisi, kwa sasa anaomba wasiiandame Yanga kwani ina mechi za kimataifa.
“Sisi tunajiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya APR tutakaocheza jumamosi, lakini jamani sisi kama Yanga tunaomba watuache wasituandame na maneno maneno, tupo katika mashindano ya kimataifa, kuhusu kuhairishwa mechi hiyo inatokana na sisi kucheza mechi za kimataifa” >>>Jerry Muro
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE