Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alisimama Bungeni Dodoma akiwataka wasanii wajiepushe kuimba siasa badala yake waelimisha jamii kauli ambayo imekuwa gumzo kwa wadau wa muziki.
Leo May 27, 2017 Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Rapa staa Kala Jeremiah ambaye amekuwa na hisia tofauti na kauli ya Waziri Mwakyembe akisema ni ngumu kuitenganisha Siasa na Muziki.
“Siasa na Muziki ni ngumu kuitenganisha kwa sababu hii kitu inaunganishwa na kitu kinaitwa Jamii. Kuna vitu vitatu; siasa, muziki na jamii na jamii inakaa katikati ya siasa na muziki.” – Kala Jeremiah.
Bonyeza Play hapa kusikiliza Full video…
Waziri Mwakyembe kuhusu Bunge Live, Davido, P Square na Tiwa Savage…