Jerry Muro ni mkuu wa idara ya habari ya club ya soka ya Yanga ambaye alizichukua headlines kuanzia magazetini juzi baada ya kusimamishwa kwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.
July 13 2016 Jerry aliandika kwenye page yake ya Instagram maneno yafuatayo >>> ‘kila nikizifikiria figisu za soka la bongo aisee nachoka kabisaa, ngoja niwe mbali kwa muda japokua nitawamiss mashabiki na watu wangu wa kimataifa’

Kama ulikua hujui ni kwamba Muro jioni ya July 7 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya maadili lilitangaza kumfungia mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 3.
Amefungiwa na kamati ya maadili kwa makosa mawili, moja alilifanya mwaka 2015 la kukaidi kulipa faini ya Tsh. milioni 5 iliyoamuliwa kulipa na kamati ya nidhamu baada ya kufanya makosa likiwa ni kosa ambalo limemfanya afungiwe mwaka mmoja kujihusisha na soka.
UMEIKOSA HII YA IDADI YA WALIOKAMATWA NA POLISI KWA KUTUMIA SHISHA DSM? BONYEZA PLAY HAPA CHINI