Jeshi la Israel, IDF awali lilisema liliharibu mahandaki 130 ya wanamgambo wa Hamas tangu mzozo huo ulipoibuka mwezi mmoja uliopita.
Kulingana na jeshi hilo, wanamgambo wa Hamas wana mtandao mkubwa wa mahandaki ya chini ya ardhi katika eneo la Ukanda wa Gaza.
IDF ilichapisha video zilizoonyesha vifaa vikichimba maeneo ya kuingia kwenye mahandaki na kuondoa vifuniko vilivyotengenezwa kwa saruji na kukuta vifaa vya kusambazia maji, hali iliyodhihirisha kwamba wanamgambo hao walikuwa wamejiandaa kukaa kwenye mahandaki hayo kwa muda mrefu. Baadhi ya mahandaki pia yalikuwa na umeme.
Mahandaki hayo yalikuwa na urefu wa mita mbili na upana wa mita moja, lakini baadhi yalikuwa na ukubwa wa kupitisha magari na yalichimbwa kwenda chini zaidi, na kuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi ya Israel.