Jeshi la Israel lilisema Jumanne kwamba limepata miili sita ya mateka ambao walipelekwa Gaza kufuatia mashambulizi ya kigaidi yanayoongozwa na Hamas Oktoba 7.
Vikosi vya ulinzi vya Israel vimesema katika taarifa yake kwamba wanajeshi waliiopoa miili hiyo katika operesheni ya usiku kucha katika mji wa Khan Younis kusini mwa Gaza.
Operesheni hiyo ilikuja wakati Marekani, Misri na Qatar zikishinikiza kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yangemaliza mashambulizi ya miezi kadhaa ya Israel huko Gaza na kuona kuachiliwa kwa mateka waliosalia kizuizini.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alionyesha matumaini siku ya Jumatatu, akisema angekuwa na mkutano “wenye tija sana” na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Alisema Netanyahu amekubali pendekezo la kuweka daraja la makubaliano ya kusitisha mapigano na kwamba “sasa ni wajibu kwa Hamas kufanya hivyo.”
Blinken aliwasili katika mji mkuu wa Misri Cairo mapema Jumanne.