Jeshi la Magereza Tanzania limesaini makubaliano na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wa mauziano ya nishati safi ambayo ni mkaa mbadala wa kupikia (Rafiki Briquettes) unaozalishwa kutokana na mabaki ya madini, lengo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu za matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mikataba hiyo imesainiwa leo katika ofisi za STAMICO Jijini Dar es Salaam ambapo umesainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhan Nyamka, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk.Venance Mwasse.
Sambamba na makubaliano hayo, pia Shirika hilo limeingia mkataba wa ushirikiano na Jeshi la magereza kwaajili ya kuendeleza utafiti na uchimbaji wa maeneo yenye leseni ya uchimbaji madini.