Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya (18) Mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi Wakuu wa Serikali Tanzania kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Tiktok.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Mtuhumiwa huyu amekamatwa Julai 29, 2023, yeye na wenzake wamekuwa wakitengeneza maudhui ya mtandaoni (video) na kuzisambasa video hizo kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha Viongozi Wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok, Mtuhumiwa huyu atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”
“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa Mtu/ Watu wanaotoa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria”