Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam imesema imejipanga kutoa ulinzi wa kutosha kwa mashabiki wa Club ya Yanga. siku ya jumamosi watakapo kabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha njia watakazo pita zipo salama na kuzuia vitendo vya uhalifu vitakavyoweza kujitokeza.
Amesema hayo kamanda wa kanda hiyo SACP Jumanne Muliro akijibu swali la waandishi wa habari lililotaka kujua kama Jeshi la Polisi kanda Maalumu lilivyojipanga kuweka ulinzi siku hiyo
“Kutokana na matangazo mengi yaliyokuwa yanafanywa na kupita raha walizonazo wahusika (mashabiki wa Yanga) sisi jeshi la polisi tunahakikisha kwanza zile njia wanazopita ziwe katika mazingira salama na wahusika wawe salama na kuona parade hilo waliloliandaa la kupita katika baadhi ya mitaa haliwi baadae na hudhuni kama baadhi ya watu wanajitoa fahamu”
“Kwahiyo jeshi litafatilia kwa karibu sheria za usalama barabarani lazima zisimamiwe, hatuta ruhusu watu kupanda pickup yenye uwezo wa kubeba watu sita ikabeba watu arobaini ni dhahiri tukiacha madhara yanaweza kutokea”