Jeshi la Polisi Nchini limeipongeza serkali ya Uturuki kwa kutoa mafunzo kwa askari wa Jeshi hilo ya namna ya kuzuia utakatishaji wa fedha haramu na kuzuia ufadhili wa ugaidi nchini Tanznia ambayo yalianza septemba 11 hadi 15 2023 katika bwalo la maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo Naibu Kamisha wa Polisi DCP Ally Lugendo amemshukuru amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anatoa dira kwa Jeshi hilo katika matumizi ya tehama na kushirikisha wataalamu wa ndani ya nchi na nje ili kuleta ufanisi katika kutoa huduma zinazoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ya sasa.
Ameongeza kuwa anamini mafunzo hayo hayo yataleta ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi na kuwajengea uwezo askari wengine ambao watapata mafunzo kutoka kwa kundi hilo la askari waliopata mafunzo kutoka Uturuki amebainisha kuwa kwakufanya ivyo Jeshi hilo litapata watalaam wengi kupitia mafunzo hayo yaliyotolewa na askari wa Jeshi la Polisi kutoka Uturuki huku akimshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kwa namna ambavyo ana waunganisha na taasisi za ndani na nje ya nchi katika kuleta matokeo Chanya ya kiutendaji ndani ya Jeshi hilo.
Kwa upande wake Mrakibu wa Jeshi la Polisi Cihan Capan Mkufunzi kutoka uturuki amesema wao kama Jeshi la Polisi kutoka uturuki wamefurahi kwa namna ambavyo askari wa Jeshi la Polisi walivyopokea mafunzo na kuonyesha ushirikiano huku akibainisha kuwa uturuki itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania katika kuboresha mafunzo kwa watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini.