Jeshi la Sudan limetoa taarifa rasmi leo asubuhi likitangaza kukubali kusitisha vita kwa muda wa masaa 72.
Mapigano ya kuwania madaraka nchini Sudan yangali yanaendelea. Ripoti ya Jumuiya ya Madaktari wa Sudan inaeleza kuwa, zaidi ya raia 427 wameuawa na wengine 700 wamejeruhiwa hadi sasa kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi na Kikosi cha Radiamali ya Haraka (RSF).
Mapigano ya silaha yalianza mjini Khartoum, mji mkuu wa Sudan, tarehe 15 mwezi huu kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan ambaye ni Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan na na kamanda wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan maarufu kwa jina la Hemedti’ Dagalo.
Televisheni ya al Jazeera imeripoti kuwa kusitishwa mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya radimali ya haraka baada ya kutekelezwa usitishaji vita. Jeshi la Sudan limekubali kusitisha mapigano kwa sharti kwamba vikosi vya RSF pia visitishe hatua zao za uhasama.
Mashambulizi ya pande mbili baina jeshi la Sudan navikosi vya RSF vimesababisha maafa na hasara kubwa kwa umma na vinatatiza huduma muhimu kama ya maji na umeme katika baadhi ya maeneo ya Sudan.