Jeshi la Sudan limesema raia 16 wa kawaida wameuawa katika shambulizi lililofanywa na kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) mjini Khartoum.
Jeshi hilo limesema kikosi cha RSF kimefanya shambulizi holela la mizinga dhidi ya makazi ya Karari na Wad al-Bakhit yaliyoko kaskazini mwa Omdurman na kaskazini magharibi mwa Khartoum, na kusababisha vifo vya watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Jeshi hilo limetoa taarifa ikisema wapiganaji pia walishambulia eneo la Al-Maseed lililoko kusini mwa Khartoum na kufyatua risasi ovyo dhidi ya raia wa kawaida na kusababisha vifo vya watu watatu.
Jeshi la Sudan limeongeza kuwa mapigano yametokea kati ya vikosi viwili katika eneo la Al-Shajara, kusini mwa Khartoum, na kusababisha vifo vya wapiganaji 5 wa kikosi cha RSF na wengine 6 kujeruhiwa.