Serikali ya Somalia imesema kuwa oparesheni mpya ya kijeshi dhidi ya kundi la al- Shabab imesababisha takribani vifo vya wanamgambo 40 katika mkoa wa Lower Shabelle.
Katika taarifa ya wizara ya habari, Utamaduni na Utalii, serikali imesema operesheni hiyo ilifanywa na jeshi la Taifa la Somalia na “Washirika wa Kimataifa” ikitaja kuhusika kwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na nchi zinaoiunga mkono jeshi la Somalia.
Oparesheni hiyo imefanyika katika viijiji vya Baldooska na Baghdad, takribani kilimenta 30 kaskazini mwa Mogadishu. Taarifa hiyo haikusema lini oparesheni hiyo ilipofanyika, lakini vyanzo vimesema ilitokea Jumatatu jioni.
Oparesheni hiyo imefanyika baada ya majeshi ya serikali kupokea taarifa kuwa wanamgambo wamekuwa wakijiandaa kufanya mashambulizi dhidi ya raia, taarifa hiyo imesema.
Chombo cha habari chenye uhusiano na Al-Shabab kimeripoti pia juu ya shambulio hilo. Na toavuti moja ya al- Shabab imedai kwamba shambulio katika kijiji cha Baghdad limeua watu 18, wakiwemo watoto saba.